Pata taarifa kuu

Côte d'Ivoire: CNS yachunguza kesi ya wanajeshi 49 waliozuiliwa nchini Mali

Nchini Côte d'Ivoire, Baraza la Usalama la Kitaifa lilifanyika Alhamisi Agosti 4. Katika kilele cha masuala yaliojadiliwa, kesi ya wanajeshi 49 wa Côte d'Ivoire waliozuiliwa Bamako kwa zaidi ya wiki tatu. Kikao cha Baraza la Usalama la Kitaifa (CNS) kiliongozwa na Alassane Ouattara, ambaye alizungumza juu ya hali hii ambayo anasema anaifuatilia "binafsi".

Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara anasema anafuatilia kesi ya wanajeshi 49 waliozuiliwa nchini Mali.
Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara anasema anafuatilia kesi ya wanajeshi 49 waliozuiliwa nchini Mali. Press Service of the Presidency/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Baraza la Usalama la Kitaifa limethibitisha kwamba maafisa wa Côte d'Ivoire, katika kesi hii maafisa wa ubalozi wa Côte d'Ivoire huko Bamako, waliweza kukutana na wanajeshi 49 waliozuiliwa tangu Julai 10 na ambao "wako salama na wanamatumaini ya kuachiliwa”.

"Baraza la Usalama la Kitaifa linasikitika, hata hivyo kuona mamlaka ya mpito ya Mali inaendelea kuwashikilia askari hawa kiholela, licha ya maelezo na ushahidi wote uliotolewa na mamlaka ya Côte d'Ivoire kuthibitisha asili ya kisheria ya kazi yao".

Alassane Ouattara anamshukuru mwenzake wa Togo Faure Gnassingbé kwa upatanishi wake na mipango yake ya "suluhisho la kidiplomasia la kwa mvutano huo kati ya Côte d'Ivoire na Mali".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.