Pata taarifa kuu

Chad: Makumi ya watu wafariki baada ya makabiliano kati ya wachimba dhahabu

Nchini Chad, makabiliano kati ya wachimba dhahabu yamesababisha vifo vya watu kadhaa huko Kouri Bougoudi kaskazini mwa nchi hiyo, karibu na mpaka wa Libya. Video kadhaa zimekuwa zikisambazwa kwa siku chache kwenye mitandao ya kijamii zikitangaza mamia ya vifo. Waziri wa Ulinzi yuko tayari kudhibiti hali hiyo.

Eneo la Tibesti kaskazini mwa Chad.
Eneo la Tibesti kaskazini mwa Chad. Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo rasmi, mapigano ya kwanza yalitokea usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii katika eneo la Tibesti, kaskazini mwa Chad. Mzozo kati ya makundi mawili ya wachimba migodi ulmezuka kati ya jamii mbili zilizotumia bunduki za kivita. Majeshi yamewasili kutoka nchi jirani ya Libya kusaidia kila jumuiya.

Kikosi cha jeshi kilichowekwa katika eneo hilo kilijaribu kuingilia kati kwa risasi za tahadhari lakini walizidiwa nguvu haraka. Katika eneo hili, kuna wachimba migodi wengi zaidi kuliko wanajeshi, kinasema chanzo cha usalama ambacho kinasema idadi ya waliofariki ni 70.

Hali ya utulivu

Jumatano hii, utulivu ulirejea mahali hapo. Ujumbe wa serikali ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi umekuwa eneo la tukio tangu Jumanne ili kurejesha utulivu na kuangalia hali katika sehemu hii ya  eneo hilo, ambalo udhibiti wake uko nje ya huduma za serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.