Pata taarifa kuu
Kenya - Uchaguzi

Kenya : Wanakandarasi wa tume ya uchaguzi wakamatwa

Tume ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, imeeleza kusikitishwa kwake kutokana na hatua ya serikali kuwakamata wanakandarasi wake watatu, wanaohusika na maandalizi ya uchaguzi wa mwezi ujao.

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Kenya, bwana Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Kenya, bwana Wafula Chebukati © Nation Kenya
Matangazo ya kibiashara

Kupitia taarifa IEBC, imesema watatu hao wafanyakazi wa kampuni ya Smartmatic International BV, walikamatwa punde baada ya kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, wakitokea nchini Venezuela.

IEBC imesema kukamatwa kwa watatu hao hakuna msingi wowote na kwamba wanakandarasi hao walisafiri hadi Kenya kuhakikisha mitambo ya electroniki itayotumiwa kwenye uchaguzi mwezi ujao, inafanya kazi bila matatizo, IEBC ikisema ilikuwa imetoa taarifa kwa vyombo vya usalama kuhusiana na ujio wa wanakandarasi hao.

Hata hivyo idara ya polisi mapema Ijumaa imetoa taarifa na kusema watatu hao wameachiliwa huru baada ya uchuguzi kukamilika.

Kenya inajianda kwa uchaguzi wa tarehe 9 mwezi ujao, ila tume ya uchaguzi imekuwa ikituhumiwa hasa na mrengo wa Azimia One Kenya Alliance, unaoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, kwamba ina njma ya kuwaibia kura wapinzani wao wa Kenya Kwanza chini ya naibu rais wa William Ruto, madai ambayo IEBC imekanusha vikali na kusema uchaguzi huo utakuwa wa huru na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.