Pata taarifa kuu
Ethiopia - Usalama

Ethiopia : Abiy aitetea serikali yake dhidi ya mauwaji ya raia

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametetea serikali yake, kuhusu madai ya kutowalinda raia waliouawa hivi karibuni baada ya kushambuliwa na wanajeshi.

 Abiy Ahmed, Waziri mkuu wa Ethiopia
Abiy Ahmed, Waziri mkuu wa Ethiopia AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza bungeni alhamisi, kiongozi huyo amewaambia wabunge kuwa serikali yake inafanya kile kilicho ndani ya uwezo wake, kuwalinda raia.

Abiy ametoa kauli huu baada mamia ya watu hasa kutoka kabila la Amhara kuuawa wiki kadhaa zilizopita, baada ya jeshi kutekeleza mashambulio mawili, katika êneo la Oromia Magharibi.

Waziri huyo mkuu wa Ethiopia amewashtumu wapiganaji wa Oromo Liberation Army, kwa kutekeleza mauaji hayo, Juni 18 na Julai 4, madai ambayo kundi hilo limekanusha.

Umoja wa Afrika umetaka uchunguzi wa kina kufanyika kubaini chanzo cha kuuawa kwa mamia ya watu , na waliohuka.

Bunge tayari limeunda Kamati maalum kuchunguza mauaji hayo na visa vingine vya ukiukaji wa  haki za binadamu vinavyofanyiwa wananchi katika nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.