Pata taarifa kuu
Ethiopia - Usalama - Siasa

Shirika la  kutetea haki binadamu nchini Ethiopia latuhumu serikali na waasi kwa kuwaua raia.

Shirika la kutetea haki za biandamu nchini Ethiopia, Ethiopian Human Rights Commission, EHRC, limetuhumu jeshi la serikali na makundi ya waasi nchini humo kwa kuwaua raia, katika taifa hilo ambalo limekuwa likishuhudia mapigano tangu mwaka 2020.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed REUTERS/Kumera Gemechu
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti ya kila mwaka EHRC, inatuhumu wanajeshi wa serikali wapiganaji wa TPLF, na wale kutoka jamii za Oromia na Amhara kwa kuhusika na mauwaji ya raia.

Ripoti hii inatolewa wakati huu serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed, ikituhumiwa kwa kuhusika na mauwaji ya waliowachache nchini Ethiopia.

Kwa mjibu wa ripoti hiyo raia waliteswa, kuawa na wengine kupotea.

Serikali nchini Ethiopia, imekatiza mawasiliano jimboni Tigray,  na kuwaacha mamillioni ya raia bila eneo hilo bila mawasiliano eneo hilo.

Katika hatua nyingine waandishi wa habari ambao wafungwa tangu mwaka uliopita idadi yao imefikia 54, 15 wakizuiliwa na vikosi vya TPLF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.