Pata taarifa kuu
Ethiopia - Usalama

Ethiopia : Hofu ya kutokea kwa mauwaji ya kimbari yaibuka

Zaidi ya mashirika 15 ya kutetea haki za bidanamu kutoka Africa, yaonya uwezekano wa kutokea kwa mauwaji ya kimbari, nchini Ethiopia, mashirika hayo yakisema mauwaji hayo huenda  yakawa sawa na yele yalitokea nchini Rwanda, iwapo umoja wa mataifa hautaingia kati na kukomesha vita vinavyoendelea.

 Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed © AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Kupitia barua ambayo mashirika hayo yameandikia baraza la usalama la umoja wa mataifa, ni kwamba uhalifu wa kivita unatekelezwa nchini Ethiopia, mbali na wahusika katika vita hivyo kutumia semi za kuchochea jamii, mfano maneno kama vile Shetani na saratani yakitumika kuwaita watu wa jamii Fulani, kama kile kilichotekea nchini Rwanda mwaka 1994.

Msharika hayo yakiongozwa na Hala Al Karib, mtetezi wa haki za wanawake kutoka pembe ya Africa, yamesema umoja wa mataifa ulipuuza hali nchini Rwanda, iliochangia kutokea kwa mauwaji hayo, na sasa hali hiyo inajitokeza tenq nchini Ethiopia.

Vita nchini Ethiopia, vianza mwezi novemba  mwaka 2020 kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa TPLF, vita hivyo vikichangia kutoke kwa hali ya kibinadamu katika jimbo la Tigray, na maeneo  jirani kama vile Amhara .

Uchuguzi wa pamoja kati ya tume ya kutetea haki za bindamu ya umoja wa mataifa na tume ya kutetea haki za binadamu nchini Ethiopia (EHRC), ulibaini kuwa pande zote katika vita hivyo, zimetekeleza uhalifu dhidi ya biandamu jimboni Tigray ikiwemo kuwaua raia na kuwateka wengine.

Kwa sasa ikadiriwa kuwa zaidi ya raia nusu millioni wamefariki kutokana na vita vinavyoendelea, wengeine millioni 4.2 wakikimbia makwao na raia millioni 9 wakihitaji msaada wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.