Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Kamati ya tuzo ya Amani ya Nobel yamtaka Abiy Ahmed kumaliza ukatili Tigray

Kamati ya tuzo ya Amani ya Nobel, imesema Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka, 2019, anawajibu mkubwa wa kumaliza umwagaji damu unaoendelea katika jimbo la Tigray.

Abiy Ahmed alitunukiwaTuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2019.
Abiy Ahmed alitunukiwaTuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2019. Amanuel SILESHI AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Berit Reiss-Andersen, amesema katia ripot yake kuwa Ahmed ana jukumu la kipekee kumaliza mzozo huo na kusaidia kurejea kwa amani, Kaskazini mwa Ethiopia.

Aidha, ameelezea masikitiko yake kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika jimbo la Tigray ambalo kwa sababu za kiusalama,misaada ya kibinadamu imekuwa haifiki katika eneo hilo.

Hali hii ya kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu, imeendelea kusababisha mamilioni yaw tau katika jimbo la Tigray kuendelea kuishi kwenye mazingira magumu kwa sababu wanakosa mahitaji muhimu kama chakula na dawa.

Kuendelea kwa mzozo wa Tigray, kumesababisha shinikizo kwa Kamati hiyo, kumpokonya Abiy tuzo hiyo, jambo ambalo hata hivyo haliwewezekani kwa kanuni za kamati hiyo.

Mzozo Kaskazini mwa Ethiopia, umekuwa ukiendelea tangu Novemba mwaka 2020 wakati wanajeshi wa serikali, walipoanza mapambano dhidi ya wapiganaji wa Tigray baada ya kuishambulia kambi za jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.