Pata taarifa kuu
Nigeria - Usalama

Nigeria : Watu wanne wafariki baada ya mlipuko

Polisi nchini Nigeria wamesema zaidi ya watu wanne wamefaraiki baada ya kutokea kwa mlipuko karibu na shule moja ya msingi, ambayo pia paa zake zimaharibiwa, katika jimbo la Kano, kaskazini mwa taifa hilo.

Baada ya kutokea kwa mlipuko nchini Nigeria
Baada ya kutokea kwa mlipuko nchini Nigeria REUTERS - NNEKA CHILE
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi wa mwanzo umeonyesha kuwa huenda mlipuko huo ulitokana na mtungi wa gesi, katika duka moja la choma vyuma, huko Sabon Gari.

Jimbo la Kano ni miongoni mwa majimbo ambayo yana idadi kubwa ya raia nchini Nigeria, na mlipuko huo umesabisha wasiwasi miongoni mwa raia kutokana na mashambulizi ya wanajihadi nchini Nigeria,  ila jimbo hilo halijakuwa likishuhudia mashambulizi mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.