Pata taarifa kuu

Wanajeshi 7 wameuawa kaskazini mwa Nigeria na watu waliojihami.

Karibia wanajeshi 7 wameuawa wengine wawili wakiwa hawajulikana waliko baada ya kushambuliwa na watu waliojihami wakati wakiwa katika shuguli yao ya kikazi katika jimbo la Taraba kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Gari la kundi la kigaidi la ISWAP Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Gari la kundi la kigaidi la ISWAP Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. AUDU MARTE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya taarifa hii vinaeleza kuwa tukio hilo la usiku wa kuamkia jumatano ya Mei 11 limetokea baada ya wanajeshi wa kikosi cha 93 kushambuliwa kwa silaha nzito wakati wakipiga doria katika kijiji cha Tati kwenye eneo la Takum mojawapo ya manispaa nchini humo.

Afisa moja wa jeshi kutoka katika kikosi hicho cha 93 ambaye hakutaka jina lake kutajwa kwa vyombo vya habari kutokana na sababu za itifaki ameeleza kuwa zoezi la kuwatafuta wenzao waliotoeka linaendelea, oparesheni ya kuwasaka waliohusika na shambulio hilo pia ikiendelea.

Hadi wakati tukichapisha taarifa hii, hakuna kundi lolote la kigaidi ambalo lilikuwa limetaja kuhusika na shambulio hilo, kundi la boko Haram limekuwa likitatiza usalama wa raia nchini Nigeria kwa muda sasa.

Mwezi jana kundi la wapiganaji wa ISWAP lilikiri kutekeleza mashambulizi mawili ya bomu katika eneo hilo la Taraba ambapo watu watatu waliuawa wengine 30 wakiaachwa na majeraha ya mwili.

Kwa zaidi ya miaka 10 sasa, usalama nchini Nigeria umekuwa ukitatizwa pakubwa na makundi ya kigaidi, mamia ya raia wakiuawa maelfu ya wengine wakiyakimbia mwakao kwa hofu ya kushambuliwa haswa katika maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo.

Mataifa jirani na Nigeria yakiwemo Niger na Chad nayo pia yamekuwa yakihangaishwa na makundi ya kigaidi, mageneg ambayo yamekuwa hata yakiwalenga wanafunzi baadhi wakitekwa na wahalifu hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.