Pata taarifa kuu
KENYA-SOKA

Muda wa kamati ya kushugulikia maswala ya soka nchini Kenya umemalizika .

Waziri wa michezo nchini Kenya Amina Mohamed amesema mwelekeo wa jinsi ambavyo maswala ya kandanda yataendelezwa kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki utajulikana siku ya alhamis ya wiki hii baada ya mashauriano na rais Uhuru Kenyatta na wadau wengine wa mchezo huo.

Waziri  wa michezo nchini Kenya, Amina Mohammed
Waziri wa michezo nchini Kenya, Amina Mohammed Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Waziri Amina amezungumza wakati akipokea ripoti kutoka kwa kamati ya muda iliyokuwa na jukumu la kusimamia maswala ya mpira nchini humo kwa muda wa miezi sita tangu kutupiliwa mbali  kwa uwongozi wa aliyekuwa rais wa shirikisho la mpira kwenye taifa hilo Nick Mwendwa.

Kamati hiyo ilikuwa chini ya uwongozi wa jaji mstaafu Aaron Ringera, kamati ambayo imekuwa ikisimamia ligi mbalimbali za mpira nchini Kenya.

Kamati hiyo inakamilisha majukumu yake zikiwa zimesalia mechi tano kabla ya kumalizika kwa mechi za msimu huu katika ligi kuu ya wanaume na wanawake, ligi zengine zikitarajiwa kumalizika mwezi ujao.

Aliyekuwa rais wa shirikisho la mpira nchini humo Nick Mwendwa, aliondolewa afisini baada ya kuhusishwa na matumizi mabaya ya ofisi.

Haijabainika iwapo kamati nyingine ya muda itaundwa kabla ya uchaguzi wa kutafuta viongozi wapya wa soka nchini humo kufanyika.

Shirikisho la kandanda duniani FIFA awali lilikuwa limeonya serikali ya kenya dhidi ya kuingilia maswala ya uwongozi wa mpira nchini kenya, taifa hilo likishikilia msimamo wake wa kutaka kusafisha shirikisho la mpira kwa manufaa ya wachezaji na mashabiki wa mpira .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.