Pata taarifa kuu

Congo Brazzaville: Paul Kagame atia saini mikataba kadhaa na Denis Sassou-Nguesso

Rais wa Rwanda Paul Kagame na Mawaziri wake wa Mambo ya Nje na Fedha wanahitimisha ziara rasmi ya siku tatu mjini Brazzaville, nchini Congo leo Jumatano. Paul Kagam na mwenzake wa Congo Denis Sassou-Nguesso wametia saini mikataba katika sekta ya uchimbaji madini, utamaduni, elimu au uchumi, hasa kwa kupeana ardhi ya kilimo cha bustani.

Paul Kagame na Denis Sassou-Nguesso wakati wa ziara ya hivi karibuni ya rais wa Rwanda nchini Congo Februari 2013.
Paul Kagame na Denis Sassou-Nguesso wakati wa ziara ya hivi karibuni ya rais wa Rwanda nchini Congo Februari 2013. AFP - LAUDES MARTIAL MBON
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili zimetia saini mikataba miwili, itifaki tatu, mikataba miwili ya maelewano na mkataba ya makubaliano katika nyanja ya kilimo. Kulingana na chanzo kinachofahamu suala hilo, Kongo imekubali kupa Rwanda hekta 12,000 za ardhi inayoweza kufanyiwa shughuli za kilimo katika angalau idara tatu kusini mwa nchi hiyo. Walakini, muda wa makubaliano haukubainishwa.

Congo ina ardhi milioni 10 hadi 12 kwa kilimo ambapo chini ya 5% inatumiwa kwa kilimo cha kujikimu.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyosomwa kwa vyombo vya habari na Jean-Claude Gakosso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo, Wakuu hao wa Nchi walizingatia kwamba kiwango cha uhusiano kati ya nchi zao kinaweza kuwa mpana na mkubwa zaidi kwa kuzingatia makubaliano yaliyotiwa saini katika siku za nyuma.

Marais wa nchi hizo mbili wamezitaka serikali zao kufanyia kazi, bila kuchelewa suala hilo, kuandaa mipango kazi ya utekelezaji wa makubaliano ambayo yamekamilika hivi punde.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.