Pata taarifa kuu
RWANDA-DIPLOMASIA

Rais wa Rwanda ziarani nchini Congo-Brazzaville

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili jijini Brazaville kwa ziara ya siku tatu. Kagame amepokelewa na mwenzake, Denis Sassou N’Guesso ambako wamefanya mazungumzo kati yao, lakini pia kujadiliana kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili. 

Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS/Eric Vidal
Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi wa nchi hizo mbili wanatarajiwa kutia saini mikataba kadhaa ya ushirikiano yenye maslahi ya nchi hizo mbili ikiwemo suala la ushirikiano wa kufanya biashara na siasa. 

Akiwa jijini Brazaville, rais Kagame anatarajiwa pia kuwahotubia wabunge na Maseneta, katika kikao cha Baraza la Congress. 

Baada ya Brazaville, rais N’Guesso atakwenda katika eneo la Oyo, jimboni Cuvette. 

Hii ni ziara inayokuja, wakati huu Congo Brazaville ikiendelea kuwapa hifadhi wakimbizi wa Rwanda wakiwemo watu wanaominiwa kushiriki kwenye mauaji ya kimbari mwaka 1994. 

Ripoti zinasema wakimbizi zaidi ya  nane sasa wanataka kupewa uraia wa Congo Brazaville. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.