Pata taarifa kuu
MALI-vikwazo

Mali: Umoja wa Ulaya wawawekea vikwazo maafisa watano akiwemo Waziri Mkuu

Umoja wa Ulaya siku ya Ijumaa umewawekea vikwazo maafisa watano wa Mali, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa mpito Choguel Kokalla Maïga, anayeshutumiwa kwa kuzuia mpito wa kisiasa katika nchi hiyo inayotawaliwa na viongozi wa mapinduzi, kulingana na taarifa.

Mbali na Waziri Mkuu, miongoni mwa maafisa waliochukuliwa vikwazo ni "wanachama wawili muhimu wa mduara wa marafiki" wa Kanali Assimi Goïta, kiongozi mkuu wa mapinduzi nchini Mali, aliyetawazwa kuwa rais wa mpito mwezi Mei 2021 baada ya mapinduzi ya pili.
Mbali na Waziri Mkuu, miongoni mwa maafisa waliochukuliwa vikwazo ni "wanachama wawili muhimu wa mduara wa marafiki" wa Kanali Assimi Goïta, kiongozi mkuu wa mapinduzi nchini Mali, aliyetawazwa kuwa rais wa mpito mwezi Mei 2021 baada ya mapinduzi ya pili. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo vinajumuisha kupiga marufuku kuingia katika nchi za  Umoja wa Ulaya na kufungia mali zao. Watu binafsi na mashirika ya Umoja wa Ulaya wamepigwa marufuku zaidi kutoa pesa kwa maafisa hawa watano.

Viongozi watano

Mbali na Waziri Mkuu, miongoni mwa maafisa waliochukuliwa vikwazo ni "wanachama wawili muhimu wa mduara wa marafiki" wa Kanali Assimi Goïta, kiongozi mkuu wa mapinduzi nchini Mali, aliyetawazwa kuwa rais wa mpito mwezi Mei 2021 baada ya mapinduzi ya pili.

Watu hao ni Malick Diaw na Ismaël Wagué, wanaochukuliwa kuwa waandaaji wa mapinduzi ya Agosti 2020, wakati ambapo jeshi lilimpindua Rais Ibrahim Boubacar Keïta, kulingana na sababu za vikwazo vilivyochapishwa katika Jarida Rasmi la Umoja wa Ulaya.

Kwa kuongezea, Ibrahim Ikassa Maïga, Waziri wa Urekebishaji Tangu Juni 2021, na Adama Ben Diarra, pia wanalengwa kwa kuwa na jukumu muhimu katika kupinduliwa kwa rais Keita, kulingana na chanzo hicho.

Maafisa hawa watano tayari wamechukuliwa vikwazo na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Hatua za ECOWAS

Mnamo Januari 9, jumuiya hiyo ilichukua hatua kali za kiuchumi na kidiplomasia dhidi ya Mali ili kukwamisha nia ya viongozi wa mapinduzi ya kusalia madarakani kwa miaka kadhaa zaidi na kukataa kwao kuandaa uchaguzi Februari 27, kama walivyojiahidi hapo awali ili kurudisha raia mamlakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.