Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UCHUNGUZI

Tume ya Zondo yachapisha ripoti yake ya 2 kuhusu ufisadi chini ya utawala wa Zuma

Ripoti mpya kutoka kwa Tume ya Uchunguzi ya Zondo iliwasilishwa kwa Raiw wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumanne Februari 1. Hii ni sehemu ya pili ya uchunguzi huu wa miaka 4 kuangazia tuhuma za ufisadi na udanganyifu ndani ya taasisi na kampuni za umma kati ya maka wa 2009 na 2018.

Jaji Raymond Zondo akiwa mkuu wa tume ya uchunguzi, hapa ilikuwa Johannesburg Aprili 20, 2018 wakati wa kusikilizwa kwa mashahidi.
Jaji Raymond Zondo akiwa mkuu wa tume ya uchunguzi, hapa ilikuwa Johannesburg Aprili 20, 2018 wakati wa kusikilizwa kwa mashahidi. GULSHAN KHAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya kwanza iliyotolewa kwa umma mwezi uliopita iliangalia hasa uporaji wa shirika la ndege la Afrika Kusini, South African Airways, na Mamalaka ya Mapato nchini Afrika Kusini. Ripoti hii mpya - yenye zaidi ya kurasa 500 - inahusiana na ubadhirifu mkubwa katika kampuni zingine 2 za serikali.

Uporaji huu uliopangwa ulilenga, kulingana na ripoti hii mpya -: kampuni ya Transnet, ambayo inasimamia reli, bandari na mabomba nchini Afrika Kusini. Baadhi ya euro bilioni 2.4 zilitolewa kinyume cha sheria na kampuni hii ya serikali kwa kampuni za marafiki wa rais wa zamani Jacob Zuma. Hasa familia ya Gupta, wafanyabiashara watatu wenye asili ya Kihindi, waliohusika katika kashfa kadhaa. Familia hii tajiri ya wazaliwa wa India ya Gupta imeshutumiwa kwa kutumia urafiki wao na rais Zuma kwa manufaa binafsi na kibiashara.

Rais huyo wa zamani pia anahusishwa katika ripoti hii kwa kuwezesha wizi wa rasilimali za umma, kwa kuwateuwa marafiki zake kwenye uongozi wa kampuni hii.

Kampuni nyingine iliyochunguzwa na tume hii ya uchunguzi, ni ile inayotengeneza silaha ya Denel, kinara wa sekta ya ulinzi na ambayo pia ilifilisishwa na mshirika wa karibu wa rais wa zamani.

Mkuu wa Nchi Cyril Ramaphosa aliitaja hati hiyo "hatua muhimu katika mapambano dhidi ya ufisadi". Ripoti ya mwisho bado itawasilishwa kwake mwishoni mwa mwezi huu. Baada ya hapo, atalazimika kuamua juu ya kesi zinazowezekana za kisheria. Lakini mashirika ya kiraia tayari yanatoa wito wa kufunguliwa kwa kesi za kisheria – hasa dhidi ya rais wa zamani Jcob Zuma – yakiamini kwamba tayari kuna ushahidi wa kutosha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.