Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-HAKI

Ripoti: Zuma alihusika na ufisadi katika utawala wake

Nchini Afrika Kusini, Tume iliyokuwa inachunguza visa vya ufisadi wakati wa uongozi wa aliyekuwa rais Jacob Zuma, imetoa sehemu ya ripoti yake baada ya miaka mitatu.

Ripoti hiyo inafuatia uchunguzi wa mahakama kuhusu ufisadi mkubwa ulioripotiwa wakati rais wa zamani Jacob Zuma akiwa madarakani.
Ripoti hiyo inafuatia uchunguzi wa mahakama kuhusu ufisadi mkubwa ulioripotiwa wakati rais wa zamani Jacob Zuma akiwa madarakani. Guillem Sartorio AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume hiyo iliyoongozwa na Jaji Raymond Zondo iliundwa mwaka 2018 kuchunguza na kubaini visa vya ufisadi wakati wa uongozi wa aliyekuwa rais Jacob Zuma, aliyekuwa madarakani kwa miaka tisa tangu mwaka 2009.

Baada ya mashahidi zaidi ya 300 kuhojiwa, Tume hiyo imEleezea kuhusu wizi wa fedha za umma ulivyofanyika katika Shirika la ndege la Afrika Kusini, lakini pia uhusiano wa karibu wa wafanyibiashara maarufu nchini humo Atul, Ajay na Rajesh Gupta ambao walikuwa wanapata mikataba mbalimbali na serikali ya Zuma.

Hata hivyo, Zuma ameendelea kukanusha madai ya kuhusika na visa vya ufisasi na hata alikataa kutoa usirikiano na Tume hiyo, na kupelekea kufungwa jela kwa kukaidi agizo la Mahakama.

Katika mapendekezo yake Tume hiyo inataka serikali kuja na mbinu za kupambana na ufisadi katika eneo la manunuzi, serikalini, kuwalinda wanaofichukua wizi wa fedha za umma na kuundwa kwa tume huru ya kupambana na ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.