Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Waasi wa Rwanda wa FDLR watoza ushuru haramu kwa wakulima wa Rutshuru

Waasi wa Rwanda wa FDLR wanashtumiwa kutoza ushuru kinyume cha sheria kwa wakulima wa DRC, hasa katika eneo la Nyamilima takriban kilomita 100 kaskazini mashariki mwa mji wa Goma, katika eneo la Rutshuru, mkoani Kivu Kaskazini. Hali hii imeendelea tangu Oktoba 2021 na ushuru huu umekuwa wa kawaida, hasa wakati wa msimu wa kilimo, kulingana na mashahidi.

Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR wakiwa kilomita 150 kaskazini magharibi mwa Goma, Februari 6, 2009.
Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR wakiwa kilomita 150 kaskazini magharibi mwa Goma, Februari 6, 2009. (Photo : Lionel Healing/AFP)
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na tovuti ya Radio Okapi nchini DRC, shuhuda zilizokusanywa Jumapili Januari 16 zinathibitisha kwamba ushuru unaoitwa "Rangira Vhuumiza" kwa Kinyarwanda au "Okoa maisha yako" ni lazima kutoa kwa wakulima ili waweze kuendesha shughuli ya kilimo kwenye mashamba yao yaliyo karibu na Nywamitwitwi, Bisoso na Nyamuragiza, kilomita 7 kutoka kijijini kwao.

Mkaazi wa Nyamilima aliyehojiwa kwa njia ya simu huko Nyamilima, alithibitisha kuwa alilipa, siku ya Ijumaa Januari 14, kiasi cha Faranga za Kongo 15,000 (7.5 USD) kwa wapiganaji hao wa FDLR, kabla ya kuingia shambani kwake, baada ya kupewa kibali ambacho hutumiwa kama risiti, kulingana Radio Okapi.

Kwa kushindwa kununua risiti hii, wakulima wanaokaidi wanapigwa vibaya, kulingana na shahidi mmoja aliyenukuliwa na Radio Okapi.

Mamlaka za utawala katika eneo hilo zinathibitisha habari hiyo. Wanaeleza kuwa wakati wa mavuno, waasi hawa hutoza ushuru kwa kila bidhaa iliyovunwa, na kwa kila mtu, kama kodi.

Vyanzo vya habari ndani ya Jeshi la DRC (FARDC) vimethibitisha hali hiyo kulingana na tovuti ya Radio Okapi.

Jeshi limetoa wito kwa wakazi wa kijiji hiki kuwa na subira. Msemaji jeshi la FARDC katika eneo hilo, Luteni Kanali Ndjike Kaiko ametoa hakikisho kwamba hatua zote zinachukuliwa ili kukomesha vitendo vya waasi hao wa Kihutu wa Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.