Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Kivu Kaskazini: kukamatwa kwa washukiwa wawili wa walipuaji huko Oicha

Idara ya ujasusi imewakamata watu wawili wanaodaiwa kutega kifaa ambacho kililipuka siku moja kabla katika soko la Oicha. Wtu hao wamekamatwa Alhamisi wiki hii (tarehe 6 Januari) kuligana na msemaji wa jeshi huko Beni, Kapteni Antony Mwalushay, ambaye amesema mlipuko huo ulisababisha watu wawili kujeruhiwa.

Oicha, mkoani Kivu Kaskazini, DR Congo: Mlinda amani akikagua pembezoni mwa kambi ya jeshi huko Oicha.
Oicha, mkoani Kivu Kaskazini, DR Congo: Mlinda amani akikagua pembezoni mwa kambi ya jeshi huko Oicha. MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Watu hawa kwa sasa wanahojiwa na idara ya ujasusi, kimehakikishia chanzo hicho.

"Kwanza kulikuwa na majeruhi wawili ambao walipelekwa hospitalini, mwanamke mmoja na mwanaume mmoja ambao walijeruhiwa kidogo. Baada ya uchunguzi wamekamatwa washambuliaji wawili ambao wanahojiwa na idara yetu ya upelelezi. Na hapo, tumepata bomu hilo kisha wataalamu wa masuala hayo wapo katika mchakato wa kufanya maelezo zaidi ili kujua zaidi chanzo na vifaa vilivyosaidia kutengenezea bomu hili la kienyeji,” amebainisha Kapteni Mwalushay.

Ameongeza kuwa hatua zimechukuliwa ili kuhakikisha usalama wa wakazi wa eneo hili.

"Katika ngazi ya kijeshi, tumeimarisha zaidi mipango ya usalama katika eneo hilo ili kuhakikisha usalama zaidi wa watu na kuwa waangalifu pamoja na watu kutoa tahadhari na kisha kuwafichua walipuaji hawa. Kuna watu wawili wamekamatwa,” ameongeza Kapteni Antony Mwalushay.

Siku ya mkesha wa Krismasi, bomu lililotengenezewa kienyeji pia lililipuka katika baa moja katika mji wa Beni, na kuua watu 8 na kujeruhi karibu 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.