Pata taarifa kuu
MALI-VIKWAZO

Baada ya vikwazo vya ECOWAS, raia wa Mali wahofia nchi yao kukabiliwa na "athari kubwa"

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilikutana katika mkutano usio wa kawaida Jumapili Januari 9 huko Accra, na kuchukuwa vikwazo vikali dhidi ya Mali.

Mwenyekiti wa ECOWAS Nana Akufo-Addo nchini Mali mnamo Mei 2021.
Mwenyekiti wa ECOWAS Nana Akufo-Addo nchini Mali mnamo Mei 2021. Nipah Dennis AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Bamako ilikuwa imependekeza kuongezwa kwa kipindi cha mpito kwa utawala wa kijeshi kwa miaka minne badala ya mitano, kipindi ambacho kilichukuliwa kuwa "kisichokubalika" na jumuiya hiyo ya kikanda Vikwazo vipya vya ECOWAS, vilivyolengwa hadi sasa dhidi ya viongozi kadhaa wa mapinduzi, ni vizito. Na wameitenga Mali.

Viongozi hao wa mapinduzi waliofanya mapinduzi mara mbilihawa kuheshimu ahadi zao za kurejea kwa utaratibu wa kikatiba hadi kufikia tarehe 27 Februari 2022; kinyume chake, wnataka kuongezwa kwa kipindi cha mpito. Aawali walitaka kuongezwa maiaka mitano na baadae wakabadili nakuomba miaka minne, matakwa ambayo yamefutiliwa mbali na ECOWAS.

Jumuiya ya Kiuchumi Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, katika mkutano wake wa siku ya Jumapili, iliidhinisha maamuzi yaliyochukuliwa na Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (WAEMU) saa chache kabla.

Nchi za Afrika Magharibi ziliamua kuzuia mali ya nchi ya Mali inayowekwa katika benki ya BCEAO, kufunga mipaka kati ya Mali na nchi wanachama wa ECOWAS lakini pia kusimamisha shughuli za kiuchumi na Bamako isipokuwa bidhaa za matibabu na muhimu. ECOWAS pia imeamua kuwaondoa mabalozi kutoka nchi zote wanachama nchini Mali pamoja na vikwazo vingine kuhusu usaidizi wa kifedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.