Pata taarifa kuu
MISRI-HAKI

Mwanaharakati Ramy Shaath aachiliwa huru baada ya kuzuiwa kwa siku 900 nchini Misri

Misri imemwachia huru mwanaharakati aliye na uraia wa nchi hiyo na Palestina, Ramy Shaath baada ya kuzuiwa kwa siku zaidi ya 900, hatua ambayo ilimlazimu kukana uraia wake wa Misri.

Shaath mwenye umri wa miaka 48, alikamatwa Juni mwaka 2019 na kuzuiwa na wanaharakati wengine, kwa madai ya kuwahifadhi magaidi.
Shaath mwenye umri wa miaka 48, alikamatwa Juni mwaka 2019 na kuzuiwa na wanaharakati wengine, kwa madai ya kuwahifadhi magaidi. FAMILY HANDOUT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka kwa familia yake imesema mwanaharakati huyo aliyekuwa mwanachama wa makundi mbali ya kisiasa na mwanzilishi wa vuguvugu linalounga mkono mamlaka ya Palestina, aliachiwa Januari 6, na kukabidhiwa kwa uoNgozi wa Mamlaka ya Palestina jijini Cairo, kabla ya kwenda Jordan.

Siku ya Jumamosi, mwanaharakati huyo amekwenda jijini Paris kuungana na familia yake. Licha ya familia yake kufurahia kuachiwa kwake huru, imeshtushtushwa na hatua ya serikali ya Misri kumlazimisha mpendwa wao kuukana uraia wake kabla ya kuachiwa.

Shaath mwenye umri wa miaka 48, alikamatwa Juni mwaka 2019 na kuzuiwa na wanaharakati wengine, kwa madai ya kuwahifadhi magaidi na mwezi Aprili mwaka 2020 alijumushwa kwenye orodha ya magaidi na watu wengine 12.

Rais Emmanuel Macron amewahi kuzungumzia kuachiliwa huru kwa mwanaharakati huyo Desemba mwaka 2020 alipokutana na rais Abdel Fattah al-Sisi jijini Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.