Pata taarifa kuu
MISRI-HAKI

Misri: Watu kadhaa wakamatwa baada ya msichana aliyenyanyaswa kujiua

Nchini Misri, watu watatu wamekamatwa na kufikishwa mbele ya ofisi ya mashtaka kufuatia kujiua kwa mwanafunzi msichana baada ya picha ya uchi ya msichana huyo wa miaka 17 iliyotengenezwa na kuchapishwa mtandaoni. Tukio ambalo liliwakasirisha watumiaji wa mtandao ambao walitaka haki itendeke.

Mwanafunzi msichana mwenye umri wa miaka 17 alidhulumiwa na vijana wawili baada ya kukataa kufanya nao mapenzi.
Mwanafunzi msichana mwenye umri wa miaka 17 alidhulumiwa na vijana wawili baada ya kukataa kufanya nao mapenzi. AFP - THOMAS COEX,-
Matangazo ya kibiashara

Bassant Khaled alijiua kwa kumeza sumu mnamo Desemba 23. Lakini wiki moja baadaye mitandao ya kijamii ilifichua suala hilo kwa kurusha barua ya kujiua ambapo Bassant alieleza kuwa hangeweza tena kuvumilia shinikizo la kijamii baada ya kuchapishwa kwa picha zao za uongo mitandaoni na vijana wawili walikuwa wakijisifu kuwa walitembea naye kimapenzi.

Shinikizo hilo halikuvumilika katika eneo la mashambani alikoishi na ambalo lilizidishwa na dhihaka za mwalimu wake mmoja ambaye pia alikamatwa.

Nambari isiyolipishwa wanaotakiwa kutumia wanawake

Washtakiwa wote watatu wanakabiliwa na kifungo hadi maisha jela. Ikiwa wazazi sasa wanamtetea binti yao, baadhi ya watumiaji wa mtandao waliwakosoa kwa kukosa uungwaji mkono huko Bassant kabla ya tukio hilo.

Baraza la Kitaifa la Wanawake, chombo rasmi, kimetangaza nambari isiyolipishwa kwa wanawake wote waathiriwa wa unyanyasaji kwenye mtandao ili kuwataja wanaohusikana vitendo hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.