Pata taarifa kuu
MALI-USHIRIKIANO

Wagner: Tangazo la washirika kumi na watano wa kimataifa lazua hisia mbalimbali

Katika taarifa ya pamoja, nchi kumi na tano za Magharibi zikiwemo Canada, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani, zinalaani kutumwa kwa mamluki kutoka kampuni ya Wagner ya Urusi nchini Mali. Uhusiano huu kati ya kampuni hii ya mamluki na mamlaka ya Bamako, uliothibitishwa na vyanzo vya RFI, unaweza kusababisha nchi nyingi zinabadili mwelekeo.

Mamluki wa kundi la wanamgambo wa Wagner katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mamluki wa kundi la wanamgambo wa Wagner katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. FLORENT VERGNES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wengi wamekuwa wakijiuluza ikiwa ni uvumi, au niukweli? Alhamisi hii, Desemba 23 huko Bamako, uthibitisho wa uwepo wa kampuni ya Urusi ya Wagner nchini Mali uliwashangaza wengi. Wengi wanahoji uwepo wa mamluki hawa kutoka Urusi kwa mujibu wa mwandishi wetu katika mji mkuu, Kaourou Magasa.

Wanasiasa wa upinzani wamelaani uwepo wa kikosi hiki cha mamluki wakibaini kwamba kinakuja kuendeleza ukatili unaodaiwa kufanywa na vyombo vya dola nchini Mali.

Fedha za umma kwa mamluki

Siku ya Alhamisi, nchi kumi na tano za Magharibi kwa hivyo zilishutumu kwa sauti moja, bila maelezo zaidi, kupelekwa kwa mamluki wa Urusi kutoka kampuni hii ya mùamluki nchini Mali: Ujerumani, Ubelgiji, Denmark, Uhispania, Estonia, Ufaransa, Italia, Lithuania, Norway, Uholanzi, Ureno. , Jamhuri ya Cheki, Rumania, Uingereza, Uswidi, na pia Canada.

Katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari, washirika hao wote wa kimataifa mjini Bamako, wanaohusika moja kwa moja au isio moja kwa moja katika mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi nchini humo, wanalaani ushiriki wa serikali ya Urusi katika kutoa msaada wa nyenzo kwa ajili ya kutumwa kwa kundi la Wagner. Ufaransa iko mbioni kurejesha Operesheni Barkhane; nchi nyingine hushiriki katika kikosi cha Takouba, au kuchangia fedha.

Kwa upande wa serikali ya Mali, hata hivyo, wanasema hakuna mkataba ambao umetiwa saini katika mwelekeo huu. Na bado, mataifa haya 14 ya Ulaya na Canada yanasikitishwa na "uamuzi wa kutumia fedha za umma kulipa mamluki wa kigeni badala ya kuunga mkono vikosi vya kijeshi vya Mali na huduma za umma".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.