Pata taarifa kuu
ETHIIOPIA-USALAMA

Ethiopia yatuhumu Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za Binadamu kutumika kisiasa

Ethiopia, imekosoa kufanyika kwa kikao maalum cha Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za Binadamu, kujadili na kuthathmini kuwepo kwa visa vya ukiukwaji wa visa hivyo katika nchi yake, kufuatia mzozo unaoendelea kati ya serikali na waasi wa Tigray.

Balozi wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa Zenebe Kebede ameishtumu Tume hiyo ambayo amesema imetekwa na fikra za kikoloni na inatumika kisiasa, Novemba 17, 2021.
Balozi wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa Zenebe Kebede ameishtumu Tume hiyo ambayo amesema imetekwa na fikra za kikoloni na inatumika kisiasa, Novemba 17, 2021. Fabrice Coffrini AFP
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa Zenebe Kebede ameishtumu Tume hiyo ambayo amesema imetekwa na fikra za kikoloni na inatumika kisiasa.

Hata hivyo, Mataifa yanayowakilishwa kwenye Tume hiyo, wametaka kutumwa kwa wachunguzi wa kimataifa kwenda kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu Kaskazini mwa Ethiopia, mzozo ambao umeendelea kwa mwezi wa 13 sasa, ambao wanahofia kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi.

Mapigano kati ya serikali ya Ethiopia na kikosi cha jeshi kutoka eneo la kaskazini la Tigray yamesababisha mzozo wa kisiasa nchini Ethiopia. Mapigano yamekuwa yakiendelea tangu Novemba 2020 na kusababisha njaa kali na vifo vya takriban watu 400,000 kufikia sasa.

Mgogoro, kung’ang’ania madaraka, uchaguzi na msukumo wa mageuzi ya kisiasa ni miongoni mwa mambo yanayochangia machafuko Ethiopia.

Historia ya siasa na uongozi Ethiopia

Nchi ya Ethiopia, rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, ni nchi ya takriban watu 117 milioni. Fasihi simulizi inaeleza kuwa utawala wa kifalme ulianzishwa na nasaba ya Solomoni kutoka kwa Mfalme Sulemani na Malkia wa Sheba chini ya mfalme wa kwanza Menelik wa kwanza.

Katika karne ya 20, Ethiopia ilikuwa taifa pekee la Kiafrika lililofanikiwa kujilinda dhidi ya ukoloni wa Ulaya, na kuishinda Italy katika vita vya Adwa. Kufuatia mapungufu ya uongozi wa kifalme pamoja na migogoro na misukosuko ya ndani, Mtawala Haile Selassie alipinduliwa mwaka wa 1974 na uongozi wa Kifalme ukakomeshwa.

Jeshi la Derg lilichukua uongozi wa nchi na kwa miaka 16, kundi la Derg na kundi la waasi kutoka Tigray na Eritrea waliongoza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 16. Mwaka wa 1987 iliunda serikali ya People’s Democratic Republic of Ethiopia iliyopinduliwa mwaka wa 1991 na Ethiopian People’s Revolutionary Democratic Front (EPRDF).

Serikali ya muungano kati ya EPRDF na vyama vingine vitatu vya kisiasa na iliyotawaliwa na kundi la TPLF ilileta mabadiliko na kuundwa kwa serikali ya shirikisho iliyojumuisha majimbo 10 ya Ethiopia.

Serikali ya muungano chini ya EPRDF ilikomeshwa mara tu Abiy Ahmed alipokuja uongozini mwaka wa 2018 kama Waziri mkuu, aliunganisha vyama tofauti vya kisiasa Ethiopia na kuunda chama cha Prosperity Party mwaka wa 2019.

Ingawa serikali ya Abiy hapo awali ilirekebisha na kukomboa siasa za nchi kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, hasa machafuko ya kikabila na uhasama kati ya serikali ya Abiy na wanachama wa TPLF yaliyochangia machafuko na mapigano katika jimbo la Tigray yaliyoanza Novemba 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.