Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Waasi wa Tigray wauteka mji wa Lalibela

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ethiopia havina uhakika zaidi kuliko hapo awali. Jeshi la shirikisho na muungano unaounga mkono serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed wamekuwa wakirejesha tena udhibiti wa eneo baada ya lingine tangu wiki mbil zilizopita, na waasi wa Tigray kulazimika kuondoka.

Kanisa la Mtakatifu George, kazi bora iliyochongwa kutoka kwenye mwamba wa volkeno ya Lalibela, katika eneo la Amhara, kaskazini mwa Ethiopia.
Kanisa la Mtakatifu George, kazi bora iliyochongwa kutoka kwenye mwamba wa volkeno ya Lalibela, katika eneo la Amhara, kaskazini mwa Ethiopia. RFI / Vincent Dublange
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni waasi wa TPLF walizindua mashambulizi mapya kaskazini mwa eneo la Amhara. Wanajeshi wa Tigray waliteka tena, Jumapili, Desemba 12, mji wa Lalibela, eneo la Urithi wa Dunia wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO.

Msemaji wa serikali Legesse Tulu hajajibu ripoti hizo za kukamatwa tena mji huo. Msemaji wa TPLF Getachew Reda pia hajatoa kauli kuhusu ripoti hizo.

Waasi walikuwa wameondoka katika mji wa Lalibela chini ya wiki mbili zilizopita kufuatia mashambulizi ya jeshi la shirikisho. Waasi wa Tigray tayari wamerejesha udhibiti wao katika mji huo, kulingana na wakazi kadhaa, Jumapili hii. Vikosi vya Ulinzi vya Tigray vinaongoza kwa mashambulizi makubwa, kulingana na makamanda wao.

Hata hivyo, walionekana wakikabiliwa na hali ngumu kwa muda wa wiki mbili, na kujiondoa kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali kufuatia mashambulizi kabambe ya muungano wa serikali, hasa ukisaidiwa na ndege zisizo kuwa na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.