Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy arejea Addis Ababa kutoka uwanja wa vita
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, amesema anarajea jijini Addis Ababa kutoka eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo amekuwa akiongoza jeshi la nchi yake kupambana na waasi wa Tigray.
Imechapishwa:
Abiy Ahmed, mwezi Novemba, alikwenda kwenye mstari wa mbele na kuacha madaraka kwa makamu wake kwa, baada ya waasi kuripoti kuchukua miji ya kimkakati na kusema wanaelekea jijini Assia Ababa.
Kiongozi huyo wa Ethiopia, anarejea Ofisini baada ya jeshi la serikali mapema wiki hii, kutangaza kupiga hatua kubwa kwa kudhibiti miji ya kimkakati ya Dessie na Kombolcha kutoka kwa waasi.
Haya yanajiri wakati huu Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika katika Pembe ya Afrika Olusegun Obasanjo, akiendelea na jitihada za kukomesha mapigano, lakini maendeleo madogo yameripotiwa kufikia sasa.
Mzozo huo unaozidi kukithiri, umechochea hofu ya uwezekano wa kusambaa katika eneo la Afrika Mashariki, huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mwezi uliopita, akizitaka pande zote mbili kuweka silaha chini.