Pata taarifa kuu

Senegal: Rais wa zamani wa shirikisho la Riadha duniani Lamine Diack aaga dunia

Rais wa zamani wa shirikisho la Riadha duniani IAAF Lamine Diack, raia wa senegal, amefariki dunia leo Ijumaa akiwa na umri wa miaka 88 nyumbani kwake nchini Senegal.

Lamine Diack rais wa zamani wa shirikisho la Riadha duniani IAAF, kuanzia mwaka 1999 hadi 2015, akiondoka katika mahakama ya Paris Juni 10, 2020.
Lamine Diack rais wa zamani wa shirikisho la Riadha duniani IAAF, kuanzia mwaka 1999 hadi 2015, akiondoka katika mahakama ya Paris Juni 10, 2020. Thomas SAMSON AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Lamine Diack alikuwa rais wa Shirikisho la Riadha duniani IAAF, kuanzia mwaka 1999 hadi 2015. Baada ya kupatikana na hatia mwaka jana kwa kosa la rushwa, Lamine Diack alihukumiwa kifungo cha miaka 4 jela na faini ya euro 500,000 kwa ufisadi wa kawaida kwa malipo ya hongo na wanariadha wa Urusi na kwa ufadhili wa kampeni za Senegal na Urusi.

Uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya mwendesha mashataka wa fedha nchini Ufaransa mwaka 2018 ni pamoja na madai kwamba Lamine Diack alichukua pesa kutoka Urusi kwa ajili ya kampeni za kisiasa za Senegal, na badala yake IAAF kusaidia kuficha makosa ya Urusi ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

Miaka michache kabla ya kuanzishwa kwa kesi hiyo, Vladimir Putin alijihusisha sana katika michezo na hasa kwenye maandalizi ya mashindano kama Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu la mwaka 2018, Michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi au Mashindano ya Dunia ya mwaka 2013 katika Riadha.

Lakini rais wa Urusi hakutaka tu kujihusisha na matukio hayo, bali pia alitaka kuona wanariadha wake wanafanya vizuri kwenye uwanja wa mashindano, alibaini Lukas Aubin, mtafiti wa jiografia na siasa, mtaalam wa masuala ya Urusi na michezo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.