Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Umoja wa Mataifa kuhamisha familia za wafanyakazi wa kimataifa kutoka Ethiopia

Umoja wa Mataifa utaziondoa ifikapo Novemba 25 familia za wafanyakazi wake wa kimataifa nchini Ethiopia, ambako mapigano yameendelea kuelekea mji mkuu, kulingana na waraka rasmi ulioandikwa Jumatatu ambao shirika la habari la AFP umepata kopi.

Wakati muungano wa waasi kutoka Tigraya na Oromo wakiwa kilomita 200 na mji mkuu wa Ethiopia, Waziri Mkuu Abiy Ahmed ametangaza kwamba atakwenda kwenye uwanja wa vita yeye binafsi kuongoza ulinzi wa mji mkuu.
Wakati muungano wa waasi kutoka Tigraya na Oromo wakiwa kilomita 200 na mji mkuu wa Ethiopia, Waziri Mkuu Abiy Ahmed ametangaza kwamba atakwenda kwenye uwanja wa vita yeye binafsi kuongoza ulinzi wa mji mkuu. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Hati hii ya ndani ya huduma ya kitengo  cha Umoja cha Mataifa inatoa wito kwa umoja huo "kuratibu zozi la kuhamisha na kuhakikisha kwamba watu wote ambao ni familia za wafanyakazi walioajiriwa kutoka ng'ambo wanaondoka Ethiopia kufikia tarehe 25 Novemba 2021 ".

Wakati huo huo Ufaransa imetoa wito kwa raia wake kuondoka nchini Ethiopia "bila kuchelewa", ambako mapigano yanakaribia mji mkuu baada ya vita vya zaidi ya mwaka mmoja kati ya vikosi vya serikali na waasi kaskazini mwa nchi hiyo.

"Raia wote wa Ufaransa wanaitwa rasmi kuondoka nchini bila kuchelewa," ubalozi wa Ufaransa mjini Addis Ababa umesema katika barua pepe iliyotumwa kwa wajumbe wa jamii ya Wafaransa waishio nchini Ethiopia.

Hayo yanajiri wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema sasa atawaongoza wanajeshi wake "kwenye uwanja wa vita."

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Ethiopia, Abraham Belay, pia amebaini kwamba vikosi vya kijeshi hatimaye vitaanza "hatua tofauti", lakini bila maelezo zaidi. "Hatuwezi kuendelea hivi," amesema kwa urahisi.

Tangu Novemba mwaka jana, serikali na vikosi vya waasi vya Tigray People’s Liberation Front (TPLF) vimekuwa vikishiriki katika vita vilivyoanzia Tigray na kuenea katika mikoa jirani ya Amhara na Afar.

TPLF limeunda muungano na vikundi vingine vya waasi likiwemo Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA) huku mzozo huo ukikaribia mji mkuu.

Jeshi la Ethiopia likiwa limedhoofika sana, vita hivi sasa vinaendeshwa katika maeneo mbalimbali hasa na wanamgambo na vikosi vya majimbo. Na juhudi za kidiplomasia za Marekani na Umoja wa Afrika zinaonekana kukwama hivi leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.