Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Mapinduzi Sudan: Ukandamizaji waua raia 40

Idadi ya vifo vya raia waliouawa katika ukandamizaji wa maandamano tangu mapinduzi ya Oktoba 25 nchini Sudan imeongezeka hadi 40 baada ya kifo cha kijana mmoja aliyejeruhiwa vibaya siku ya Jumatano na kufariki dunia Jumamosi hii, kulingana na idadi mpya ya vifo kutoka chama cha madaktari.

Waandamanaji wanaopinga mapinduzi wakikabiliana na vikosi vya usalama huko Khartoum, Sudan.
Waandamanaji wanaopinga mapinduzi wakikabiliana na vikosi vya usalama huko Khartoum, Sudan. - AFP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo tarehe 25 Oktoba, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, mkuu wa jeshi na kiongozi mkuu wa mapinduzi, ameendelea kuchukua hatua kadhaa za kukabiliana na waandamanaji wanaopinga mapinduzi hayo kwa miezi kadhaa nchini Sudan. Amewakamata raia wote waliokuwa madarakani, akasitisha muungano mtakatifu ulioundwa na raia na askari na kutangaza hali ya hatari.

Tangu wakati huo, maandamano dhidi ya jeshi na kutaka kurejeshwa kwa mamlaka ya kiraia yamefanyika hasa mjini Khartoum, na mara nyingi yamekandamizwa na vikosi vya usalama.

Jumatano Novemba 17 ilikuwa siku mbaya zaidi kwa vifo vya watu 16, wengi wao wakiwa waliuawa huko Khartoum-Kaskazini, kitongoji kinachounganishwa na mji mkuu na daraja la mto Nile, kulingana na muungano wa madaktari wanaounga mkono demokrasia. Mmoja wao aliyepigwa risasi siku hiyo alifariki dunia Jumamosi hii.

"Mvulana mwenye umri wa miaka 16 aliyejeruhiwa vibaya na majeraha ya risasi kichwani na mguuni Novemba 17 amekufa kama shujaa," chama cha madaktari kimesema katika taarifa.

Kifo hiki kinafikisha idadi ya watu 40, wakiwemo vijana, waliouawa wakati wa maandamano tangu Oktoba 25. Idadi kubwa ya watu waliouawa ni waandamanaji.

Polisi wanahakikisha kwamba hawajawahi kuwafyatulia risasi waandamanaji na kubaini kifo kimoja tu na watu 30 kujeruhiwa kati yao kutokana na gesi ya kutoa machozi, dhidi ya polisi 89 waliojeruhiwa.

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Alhamisi alilaani ukandamizaji huo na kuwataka wanajeshi kuruhusu maandamano ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.