Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Madereva 72 wa shirika la Umoja wa Mataifa (WFP) wazuiliwa Ethiopia

Ethiopia inawashikilia madereva 72 wa shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika mji wa kaskazini ulioko kwenye barabara pekee inayotumiwa kwa kusafirisha misaada ya kibinadamu kuingia Tigray, Umoja wa Mataifa umesema Jumatano hii, huku kukiwa na msukosuko wa juhudi za kidiplomasia kukomesha mzozo huo ambao umedumu kwa mwaka mmoja.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alikuwa ameahidi ushindi wa haraka.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alikuwa ameahidi ushindi wa haraka. EDUARDO SOTERAS AFP/File
Matangazo ya kibiashara

“Tunathibitisha kuwa madereva 72 walioajiriwa na shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wanazuiliwa Semera. Tunawasiliana na serikali ya Ethiopia ili kuelewa sababu za kuzuiliwa kwao, "amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa.

Awali shirika la habari la AFP likinukuu vyanzo vya Umoja wa Mataifa na kibinadamu, liliripoti kuwa watu zaidi ya 10 walikamatwa wakati wa operesheni zilizowalenga watu wa jimbo la Tigray kama sehemu ya hali ya hatari inayoendelea nchini Ethiopia.

"Baadhi yao walikamatwa wakiwa majumbani mwao," kiliongeza moja ya vyanzo vya AFP. 

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu 400,000 katika jimbo la Tigray wanakabiliwa na kitisho cha baa la njaa.

Wakati huo huo Umoja wa Afrika na Marekani wamesema wanaona kuna nafasi ndogo ya fursa ya vita vya Ethiopia kumalizwa, wakati Umoja wa Mataifa ukitahadharisha juu ya nchi hiyo kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.