Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Abiy Ahmed atangaza vita dhidi ya waasi wa TPLF

Nchini Ethiopia, waasi wa TPLF wanaonekana kuendelea kusonga mbele katika eneo la Amhara. Mapigano yanaendelea katika mji wa Dessie na viunga vyake. Waasi wa TPLF waliingia katika mji huo wenye wakaazi 200,000 siku ya Jumamosi, lakini inaripotiwa kuwa bado hawajadhibiti kikamilifu mji huo. Katika harakati hizo, waliingia pia katika mji mkubwa jirani wa Kombolcha.

Watu wakitembea kando ya barabara nje kidogo ya mji wa Dessie, Ethiopia, Desemba 13, 2020.
Watu wakitembea kando ya barabara nje kidogo ya mji wa Dessie, Ethiopia, Desemba 13, 2020. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abby Ahmed amesema katika taarifa kuwa wanajeshi wa serikali kuu wanapambana katika maeneo matatu dhidi ya wanajeshi wa Tigray akiwaambia wafuasi wake kuwa nguvu kubwa za adui zinatokana na udhaifu na kutojiandaa kwa serikali. Amewahimiza wafuasi wake kuongeza juhudi maradufu katika vita vya nchi hiyo

Addis Ababa inatiwa wasiwasi na kuendelea kusonga mbele kwa waasi hao katika kipindi cha siku tatu zilizopita. Jumapili jioni, serikali ilikanusha kutekwa kwa miji hiyo miwili ikisema kuwa "mapigano makali" yalikuwa yanaendelea.

Hali ya kijeshi bado haijafahamika katika eneo hili la Wollo, lililoko kilomita 400 kaskazini mwa Addis Ababa. Ikiwa inajulikana kuwa waasi wa TPLF wameingia katika miji miwili mikuu ya eneo hilo, Dessie na Kombolcha, ni vigumu kujua ikiwa wana udhibiti kamili ya miji hiyo, hasa kutokana na kukatwa kwa mawasiliano ya simu.

Pia ni vigumu kukadiria uwezo wa jeshi la shirikisho, ambalo lilidai kuanzisha mashambulizi makubwa kukabili waasi  wa TPLF.

Serikali ya Ethiopia Jumapili ilikanusha madai ya waasi wa TPLF kuteka miji miwili ya kimkakati kaskazini mwa nchi hiyo, ikisema wanajeshi wake bado wanapigania udhibiti wa eneo hilo. "Kwa sasa kuna mapigano makali kwenye pande za Dessie na Kombolcha," msemaji wa serikali Legesse Tulu alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.