Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Mvutano wa kisiasa Somalia: Rais na waziri mkuu wafikia makubaliano

Nchini Somalia, huu unaweza kuwa mwisho wa mzozo wa kisiasa ambao umedhoofisha mamlaka ya utendaji katika miezi ya hivi karibuni: Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, akijulikana kwa jina maarufu Farmajo, na Waziri wake Mkuu Mohammed Hussein Roble wamefikia makubaliano ya kumaliza tofauti zao.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, anayejulikana kwa jina maarufu Farmajo.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, anayejulikana kwa jina maarufu Farmajo. Yasuyoshi CHIBA AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Maelewano ya Alhamisi yanatarajiwa kuwezesha nchi hii kufanyika kwa uchaguzi wa urais katika hali utulivu, ambao ni muhimu kwa mustakabali wa nchi.

Wawili hao walionana jioni katika ikulu ya rais wa Somalia huko Mogadishu, Villa Somalia. Walikuwa tayari walionana siku moja kabla, pia jioni, bila kutolewa kwa taarifa baada ya mazungumzo yao ya kwanza kwa wiki kadhaa.

Lakini wakati huu, upatanisho wao umetangazwa rasmi. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa ikulu ya rais ameelezea kufanyika kwa makubaliano kati ya rais wa Somalia na waziri wake mkuu. Waziri wa Usalama wa Ndani Abdullahi Mohamed Nour, aliyeteuliwa na Waziri Mkuu, bado yuko katika wadhifa wake. Kama ilivyo kwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi Yassin Farah, aliyeteuliwa na rais.

Baada ya wiki kadhaa za mvutano na vitisho, maelewano haya yamesafisha hali ya kisiasa, wakati mchakato wa kumchagua rais mmoja kwa moja unaendelea, baada ya kuchelewa kwa wiki kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.