Pata taarifa kuu
ICJ-HAKI

ICJ: Somalia yapata ushindi dhidi ya Kenya kuhusiana na mpaka wa baharini

Somalia na Kenya zimekuwa zikipambana tangu 2014 katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kutatua mizozo kati ya mataifa.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo akutanakwa mazungumzo na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta jijini Nairobi Machi 23, 2017.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo akutanakwa mazungumzo na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta jijini Nairobi Machi 23, 2017. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Eneo la mpaka wa baharini kati ya nchi hizo mbili na rasilimali ya gesi na mafuta katika eneo la mita za mraba 100,000 ndio eneo lnalozozaniwa.

Majaji walitoa uamuzi kuhusu mpaka wa usawa wa bahari, kama ilivyodaiwa na Somalia, wakati wakibadilisha kidogo mchoro wa mpaka huo kwa manufaa ya Kenya. Majaji, hata hivyo, walikataa madai ya Somali kulipwa fidia.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Somalia  mwaka 2014 ikidai kuwa jirani yake Kenya ilikuwa imechukua sehemu ya bahari yake, suala ambalo limesababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Somalia ilikuwa inataka mpaka huo wa majini kuchorwa upya, kwa kufuata mpaka ya ardhini ,huku Kenya ikidai kuwa tangu mwanzo imekuwa ikichukua mkondo wa mstari wa usawa,

Mwezi Machi, Kenya ilijiondoa kwenye kesi hiyo, kwa kile ilichoeleza kuwa, Mahakama hiyo ilikuwa na upendeleo kuhusu eneo hilo lenye mzozo, ukubwa wa Kilomita 160,000 katika bahari ya Hindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.