Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Mapigano yanayohusisha waasi wa Chad yaripotiwa kusini mwa nchi Libya

Mapigano kati ya waasi wa FACT na wanajeshi wa Chat wakisaidiwa na vikosi vya Khalifa Haftar yalifanyika Jumanne, Septemba 14, 2021, kulingana na taarifa kutoka waasi wa Chad, wa FACT, Front for Alternation and Concord in Chad, kundi la waasi lililodai kuhusika na kifo cha Idriss Déby Itno mnamo Aprili.

Vikosi vya LNA vinavyomtii Khalifa Haftar vikiwa karibu na Obari, kusini mwa Libya.
Vikosi vya LNA vinavyomtii Khalifa Haftar vikiwa karibu na Obari, kusini mwa Libya. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mashambulio ya angani yaliyofanywa na vikosi vya Khalifa Haftar yalilenga kambi moja ya kundi la waasi wa Chad katika eneo hili la jangwa.

Shambulio la kwanza la bomu liliripotiwa kuanza karibu saa nne asubuhi Jumanne, likifuatiwa na la pili jioni, karibu na Tarbou kusini mwa Libya.

"Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yalitekelezwa katika eneo hilo," amesema msemaji wa kundi la waasi, Kingabé Ogouzeïmi De Tapol. Ameongeza kuwa mashambulizi haya yalilenga Mahamat Mahdi Ali.

Mkuu wa kundi hilo la waasi la FACT, ambaye anaongoza mashambulizi katika uwanja wa vita, amethibitisha vifo vya waasi saba wa Chad, ikiwa ni pamoja na makada watano. Ametaja makumi ya vifo kwa upande wa Libya. Vikosi vya Khalifa Haftar vimekiri kutekeleza mashambulizi hayo. Lakini serikali ya Chad imekanusha kuwepo kwa asjkari wake katika ardhi ya Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.