Pata taarifa kuu
LIBYA-HAKI

Libya: Saadi, mtoto wa kiongozi wa zamani Muammar Gaddafi, aachiliwa huru

Saadi Kadhafi, mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Kadhafi, aliyekuwa akizuiliwa jela katika mji mkuu Tripoli tangu mwaka 2014, ameachiliwa huru kulingana na uamuzi wa mahakama, Wizara ya Sheria ya Libya imesema.

Saadi Gaddafi, 47, alikuwa alikimbilia nchini Niger wakati baba yake alipinduliwa kabla ya kupelekwa Libya mnamo 2014. Alikuwa kizuizini huko Tripoli tangu wakati huo.
Saadi Gaddafi, 47, alikuwa alikimbilia nchini Niger wakati baba yake alipinduliwa kabla ya kupelekwa Libya mnamo 2014. Alikuwa kizuizini huko Tripoli tangu wakati huo. REUTERS/Tim Wimborne
Matangazo ya kibiashara

"Saadi Mouammar Gadhafi ameachiliwa huru, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa mahakama" uliyotolewa miaka kadhaa iliyopita, chanzo kutoka Wizara ya Sheria kimeliambia shirika la habari la AFP.

Jumapili jioni vyombo vingi vya habari nchini Libya vimeropiti kuwa Saadi Gaddafi tayari alikuwa ameondoka nchini Libya kwa ndege kuelekea Uturuki.

Kulingana na shirika la habarila AFP, chanzo kutoka ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu kimesema mtoto wa Gaddafi alikuwa ameachiliwa kwa pendekezo la mwendesha mashtaka. "Mwanasheria Mkuu alikuwa ameomba, miezi kadhaa iliyopita, kutekelezwa kwa uamuzi juu ya kuachiliwa kwa Saadi Gaddafi mara tu masharti yote yatakapotimizwa," chanzo hiki kimesema, na kuongeza kuwa yuko "huru kubaki nchini au kwenda nje ya nchi".

Saadi Gaddafi, 47, alikuwa alikimbilia nchini Niger wakati baba yake alipinduliwa kabla ya kupelekwa Libya mnamo 2014. Alikuwa kizuizini huko Tripoli tangu wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.