Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Rais mteule wa Zambia afanya mageuzi katika jeshi na polisi

Rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema amewateua viongozi wapya wa Jeshi nchini humo na kuteuwa Makamishena wapya wa Polisi, hatua inyaokuja baada ya kuapishwa wiki iliyopita.

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kuchaguliwa kwake, Agosti 2021.
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kuchaguliwa kwake, Agosti 2021. © Tsvangirayi Mukwazhi/AP
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake baada ya kuapishwa wiki iliyopita, rais Hichilema aliahidi kumaliza kile alichosema ni dhuluma kwa raia iliokuwa unatekelezwa na maafisa wa usalama.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalikuwa yanaishtumu serikali iliyopita ya kiongozi wa zamani Edgar Lungu kwa kuwahangaisha wapinzani, kwa kuwakamata mara kwa mara akiwemo rais wa sasa.

Hata hivyo, rais Hichilema hakusema ni kwanini amefanya mabadiliko hayo lakini ameagiza kuwa, maafisa wa polisi wasiwakamate watu nchini humo bila ya uchunguzi.

Hichilema alipata ushindi mkubwa wakati wa uchaguzi wa mwezi huu na amekuwa akiahidi kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini humo na kuheshimu haki za wapinzani.

Wakati akiwa kwenye upinzani, Hichilema alikamatwa na kuzuia mara kadhaa kufuatia harakati za kutafuta uongozi wa taifa hilo ya Kusini mwa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.