Pata taarifa kuu
ZAMBIA-UCHUMI

Zambia: rais mpya Hakainde Hichilema akabiliwa na changamoto za kiuchumi

Baada ya kushinda uchaguzi kwa kura milioni 2.8 kulingana na matokeo ya mwisho ya duru ya kwanza, Hakainde Hichilema amechaguliwa kuwa rais wa 7 wa Jamhuri ya Zambia.

Rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema wakati wa hotuba yake kwa vyombo vya habari kwenye makazi yake huko Lusaka Jumatatu, Agosti 16, 2021.
Rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema wakati wa hotuba yake kwa vyombo vya habari kwenye makazi yake huko Lusaka Jumatatu, Agosti 16, 2021. © Tsvangirayi Mukwazhi/AP
Matangazo ya kibiashara

Wazambia wamempigia kura mfanyabiashara huyo, anayejulikana kama "HH", kwa sehemu kubwa kwa ahadi yake ya kufufua uchumi. Kuanzia sasa, rais huyo mpya atalazimika kukidhi matarajio ya wapiga kura.

"Uchaguzi huu ulikuwa kura ya maoni kuhusiana na uchumi," Nicole Beardsworth, muhadhiri wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini, ameiambia RFI. Zambia, nchi ya kusini mwa Afrika yenye watu milioni 17, inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi. Asilimia 60 ya raia wanaishi katika umaskini mkubwa, kulingana na Benki ya Dunia, na wanashindwa kukidhi mahitaji yao.

"Wapiga kura waliokuwa wakisubiri kwenye foleni katika vituo vya kupigia kura walisema hawawezi hata kuolewa kwa sababu wanaume hawana na pesa za kulipa mahari. Kwa hivyo wasichana ambao nilizungumza nao walisema watampigia kura Hakainde Hichilema ili kupata waume, ”anasema mtaalam huyo, ambaye alikaa wiki tano huko Lusaka akiongoza mtandao wa utafiti kuhusiana na uchaguzi wa urais.

Zambia yakabiliwa na mzigo wa madeni

Hata hivyo Beardsworth anahofia kuwa ahadi za rais mteule huenda zisitekelezwi

"Wazambia waliweka imani yao kwake kubadili haraka uchumi. Hii inaweza kuwa mtego, amebaini mtaalamu huyo. Ninahofia uzito wa matarajio haya ambayo ni mzigo mkubwa kwake. "Hakainde Hichilema atalazimika kushughulikia miradi kadhaa ambayo ni kipaumbele ili kuleta marekebisho nchini Zambia, hasa kupunguza deni.

Zambia, mzalishaji wa pili mkubwa wa shaba Afrika, inadaiwa zaidi ya dola bilioni 12 na wadai wa kigeni. Zambia inakuwa taifa la kwanza barani Afrika, wakati huu wa mlipuko -kushindwa kulipa deni mwezi Novemba wakati ambao itaacha kulipa riba kwa kutumia mikopo mingine.

Wakati wa kampeni, Hakainde Hichilema alimkosoa mpinzani wake kwa kutegemea sana miundombinu na sio kuwekeza vya kutosha katika tija. Kampuni za China zilichangia zaidi ya 80% kwa miradi ya ujenzi wa Zambia, kwani mfumuko wa bei uliongezeka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.