Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Ishirini na nne waangamia katika shambulizi la wanajihadi

Wanajeshi 24 wa Chad wameuawa kufuatia shambulizi lililotekelezwa na wanajihadi katika eneo la Ziwa Chad, kwa mujibu wa uongozi wa jeshi nchini humo.

Gari la jeshi la Chad huko Koundoul, kilomita 25 kutoka Ndjamena.
Gari la jeshi la Chad huko Koundoul, kilomita 25 kutoka Ndjamena. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi Jenerali Azem Bermandoa Agouna, amethibitisha kuwa shambulizi hilo lilitokea katika eneo la Tchoukou Telia, Kilomita 190 kutoka jiji kuu N'Djamena, hata hivyo hakutoa idadi ya wanajeshi waliouwa.

Hata hivyo, kiongozi wa eneo hilo Haki Djiddi, amesema wanajeshi hao walishambuliwa na wanamgambo wa Boko Haram wakati wakitoka kupiga doria.

Mbali na mauaji ya wanajeshi hao 24, wengine ambao idadi yao haijafahamika, walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Eneo la Ziwa Chad linapakana na mataifa ya Niger, Nigeria na Cameroon na kwa kipindi kirefu, limeendelea kushuhudia utovu wa usalama kutokana na kuwepo kwa kundi la Boko Haram.

Mwezi Machi mwaka 2020, karibu wanajeshi wengine 100 wa Chad waliuawa katika eneo la Bohoma. Mwezi Aprili mwaka huu, rais Idriss Deby Itno aliauwa kwenye mapambano ya vita, Kaskazini mwa nchi hiyo, kulingana na taarifa ya serikali ya nchi hiyo wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.