Pata taarifa kuu
ETHIIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Vita vya Tigray vyatishia kuenea katika maeneo mengine ya nchi

Nchini Ethiopia, Waasi wa Tigray tayari wameanzisha mashambulio dhidi ya eneo jirani, mkoa wa Amhara. Baada ya wito kutoka kwa Waziri Mkuu, majimbo mengine ya Ethiopia yanakusanya wanajeshi wao.

Uharibifu uliosababishwa na vita kati ya vikosi vya serikali ya Ethiopia na waasi wa TPLF huko Tigray.
Uharibifu uliosababishwa na vita kati ya vikosi vya serikali ya Ethiopia na waasi wa TPLF huko Tigray. © RFI/Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya waasi huko Tigray vinasema wameanzisha shambulio katika mkoa mwingine kuzuia kuwasili kwa wanajeshi zaidi wa serikali.

Ni operesheni ndogo iliyofanywa na waasi wa Tigray katika mkoa wa Afar, kulingana na mmoja wa wasemaji wake.

Lengo rasmi ni kuzuia vikosi maalum kutoka sehemu nyingine ya Ethiopia, husuna katika jimbo la Oromia. Kwa sababu kwa ombi la serikali ya Ethiopia, majimbo kadhaa yamepeleka vikosi vyao maalum kwenye mpaka na jimbo la Tigray. Kuna askari kutoka Oromia, lakini pia kutoka Sidama, mkoa wa Somali na mkoa wa kusini.

Maelfu ya wanajeshi wa ziada wanakuja kusaidia jeshi la shirikisho, lakini pia vikosi maalum na wanamgambo wa Amhara ambao hujikuta katika mstari wa mbele.

Waasi wa Tigray, kwa hivyo, wanatafuta zoezi hilo kubwa katika mkoa wa Afar, hali ambao inaongeza sintofahamu katika jimbo la Tigray. Kwa sababu tayari mapigano yanafanyika kusini na magharibi mwa jimbo hilo.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwa mara nyingine ametoa wito wa mshikamano wa kitaifa kukabili chama cha TPLF, ambacho, kwenye akaunti yake ya Twitter, alikiita "saratani".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.