Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Ethiopia: Majimbo kadhaa kushirikiana na serikali kuu katika vita dhidi ya waasi

Uongozi wa majimbo matatu nchini Ethiopia yakiongozwa na yale ya  Oromia na Sidama, yametangaza kuwa tayari kushirikiana na vikosi vya serikali kuu, kupambana na waasi katika jimbo la Tigray, baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuonya kuwa, jeshi la nchi hiyo linaweza kurejea tena katika jimbo hilo.

Wapiganaji wa kundi la TDF katika mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele.
Wapiganaji wa kundi la TDF katika mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele. Yasuyoshi Chiba AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, msemaji wa Kamati ya serikali inayoshughulikia mzozozwa Tigray, Redwan Hussein ameyashtumu baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kuwaapa waasi silaha.

Mzozo ambao umetokea kwa zaidi ya miezi nane, kukiripotiwa ukatili na pia kuongezeka kwa njaa, ulichukuwa sura mpya mwishoni mwa mwezi Juni wakati waasi walipopata udhibiti wa sehemu kubwa ya jimbo la Tigray, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa jimbo hilo, Mekele, na kupelekea serikali kutangaza kusitisha vita.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed alizindua operesheni ya kijeshi Novemba 4 kuwatimuwa na kuwapokonya silaha viongozi wa jimbo la Tigray walioasi kutoka kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF).

Serikali ilitangaza ushindi baada ya kudhibiti mji wa Makele Novemba 28, ikiungwa mkono na wanajeshi kutoka Eritrea jirani na mkoa wa Amhara. Lakini mapigano yakaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.