Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali yasimamishwa uanachama wa Umoja wa Afrika

Baada ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Umoja wa Afrika umechukuwa uamuzi wa kusimamisha uanachama wa Mali.

Kanali Assimi Goita, aliyejitangaza kiongozi wa mpito Mali.
Kanali Assimi Goita, aliyejitangaza kiongozi wa mpito Mali. ANNIE RISEMBERG AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa jana usiku, Baraza la Amani na Usalama linataka kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba na kuwataka wanajeshi kurudi katika kambi zao.

AU inataka uteuzi wa raia kuongoza kipindi cha mpito pamoja na kuachiliwa kwa wale wote waliokamatwa wiki iliyopita.

Umoja wa Afrika pia umesema hautapendelea kiongozi yeyote wa mpito kuwania kwenye nafasi yoyote katika uchaguzi ujao.

AU imebainisha kuwa inaweza kuweka vikwazo dhidi ya watu watakaosababisha "machafuko yatakayo fanywa katika kipindi cha mpito".

Wiki iliyopita, Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi zilichukua hatua kama hii, wakati huu kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita akiahidi kuandaa uchaguzi mwaka ujao na kukabidhi madaraka kwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.