Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali yasimamishwa uanachama wa ECOWAS baada ya jaribio la mapinduzi

Viongozi wa jumuiya ya kiuchumi wa nchi za Afrika magharibi ECOWAS, wametangaza kusitisha uanachama wa nchi ya Mali katika jumuiya hiyo kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliotokea mara mbili ndani ya kipindi cha miezi tisa. 

Kanali Assimi Goïta, sasa rais wa mpito wa Mali, kwenye mkutano wa ECOWAS huko Accra,  Septemba 2020 (Picha ya zamani)
Kanali Assimi Goïta, sasa rais wa mpito wa Mali, kwenye mkutano wa ECOWAS huko Accra, Septemba 2020 (Picha ya zamani) REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya kikao cha viongozi wa mataifa 10 wa Jumuiya hiyo jijini Accra nchini Ghana, kuthathmini mchakato wa kipindi cha mpito na kushinikiza viongozo wa kijeshi nchini Mali kuunda serikali shirikishi chini ya waziri mkuu ambaye atakuwa ni raia, huku wakiwataka viongozi wa nchi hiyo  kuzingatia kalenda ya kipindi cha mpito.

Katika tamko la mwisho viongozi wa ECOWS wamesema wana wasiwasi mkubwa na hali ya usalama kwenye eneo la Afrika Magharibi kutokana na kile kinachoendelea nchini Mali.

Kupitia taarifa kuhusu maazimio ya mkutano huo iliyowasilishwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Ghana Shirley Attorkor uanachama wa Mali utasitishwa hadi Februari 2022 ambao ni muda uliopangwa kwa taifa hilo kufanya uchaguzi na madaraka kukabidhiwa kwa serikali ya kiraia itakayochaguliwa kidemokrasia.

Mbali na hayo, viongozi wa kipindi cha mpito, waziri mkuu, rais na makamu wa rais watatakiwa kukaa kando baada ya kipindi cha mpito na kutowania nafasi yoyote kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.