Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali: Rais Bah N'Daw na Waziri Mkuu Moctar Ouane wajiuzulu

Rais wa Mali Bah N'Daw na Waziri Mkuu Moctar Ouane wametangaza kujiuzulu Jumatano hii, Mei 26 mapema alasiri. Ujumbe wa pande tatu, unaoundwa na wawakilishi wa ECOWAS, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, huko katii, ambapo viongozi hao wawili wa Mali wanashikiliwa tangu kukamatwa kwao Jumatatu, Mei 24.

Rais wa kipindi cha mpito Bah N'daw na Waziri Mkuu Moctar Ouane wametangaza kujiuzulu.
Rais wa kipindi cha mpito Bah N'daw na Waziri Mkuu Moctar Ouane wametangaza kujiuzulu. © REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili wa Mali wanaozuiliwa na viongozi wa mapinduzi (CNSP) katika kambi kuu ya jeshi tangu Jumatatu alasiri , wamepokea leo asubuhi ujumbe waJumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Umoja wa Afrika na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma), ukiongozwa na mpatanishi wa ECOWAS Goodluck Jonathan.

Timu ya upatanishi imekuwa ikijaribu tangu jana (Jumanne) kutafuta njia ya kutoka kwa mgogoro ambao Mali inapitia tangu mapinduzi mapya ya wanajeshi wa CNSP, wasio na furaha na serikali mpya iliyotangazwa Jumatatu, ambapo maafisa wawili wa jeshi hawakurejeshwa kwenye nafasi zao walizokuwawakishikilia katika serikali ya awali.

Kanali Goïta alisema Jumanne jioni kwamba alikuwa amewafuta kazi viongozi hao wawili akiwashhtumu kuunda serikali mpya bila kushauriana naye wakati ni makamu wa rais anayesimamia maswala ya usalama.

Rais Bah N'Daw na Waziri Mkuu Moctar Ouane wametangaza kujiuzulu wakati ujumbe huo wa pande tatu ulipowasilikatika kambi ya Kati wanakozuiliwa. "Tulipofika, walisoma barua yao ya kujiuzulu ambayo ilikuwa tayari imeandikwa," kilisema chanzo cha kidiplomasia cha Afrika Magharibi, kilichoshiriki kwenye mkutano huo leo asubuhi. Chanzo hiki kimebainisha kuwa hakufurahishwa na utaratibu uliotumiwa. “Hatuwezi kukana kwamba walijiuzulu kwa kulazimishwa. "

Assimi Goïta atachukua nafasi ya rais

Muda mfupi kabla ya kumalizika kwa mkutano huo, habari za kujiuzulu kwa viongozi hao wawili walioteuliwa ilivujaa, na kuthibitishwa na wasaidizi wa viongozi wa mapinduzi. Kulingana na chanzo hicho cha kidiplomasia, mkuu mapinduzi ambaye pia ni makamu wa rais wa sasa Assimi Goïta ametangaza mpango wake wa siku zijazo: atachukua nafasi ya rais wa mpito, na wadhifa wa makamu wa rais utabaki wazi. Kuhusu nafasi ya Waziri Mkuu, hakuna maelezo yoyote yalitolewa lakini inajulikana kwamba mashauriano yalianza Jumatatu, hasa na vuguvugu la M5.

Kwa upande wa rais wa sasa na waziri mkuu wa zamani, wanatarajiwa kuachiliwa leo jioni, ikiwa ni pamoja na wafungwa wengine wanaohikiliwa pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.