Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Ethiopia kufanya uchaguzi Juni 21

Uchaguzi Mkuu nchini Ethiopia sasa umeratibiwa kufanyika tarehe 21 mwezi Juni, siku 16 zaidi kama ambavyo ilikuwa imepangwa hapo awali.

Wakimbizi wa nadani waliopewa hifadhi kwenye jengo karibu na Chuo Kikuu cha Aksum, katika mji wa Shire, huko Tigray, Machi 14, 2021.
Wakimbizi wa nadani waliopewa hifadhi kwenye jengo karibu na Chuo Kikuu cha Aksum, katika mji wa Shire, huko Tigray, Machi 14, 2021. REUTERS - BAZ RATNER
Matangazo ya kibiashara

Tarehe hii mpya imetangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo, na sasa hii ni mara ya pili kwa uchaguzi nchini humo, kucheleweshwa.

Uchaguzi Mkuu nchini Ethiopia ulikuwa umepangwa kufanyika mwaka uliopita, lakini ukaahirishwa kwa sababu ya janga la Covid 19.

Ucheeleweshwaji huo ulizua mvutano wa kisiasa nchini humo huku wapinzani wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed wakimthumu kutumia janga la Corona kama njia ya kuendelea kusalia madarakani.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi wiki iliyopita, ilitanagaza kuwa, kulikuwa na changamoto kwenye maandalizi ya uchaguzi huo pamoja na usajili wa wapiga kura, suala ambalo lilichangia ucheleweshwaji wa uchaguzi huyo.

Uchaguzi katika jimbo la Tigray, ambalo linashuhudia utovu wa usalama umeahirishwa hadi itakapotangazwa amri mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.