Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Abiy Ahmed ataka uchaguzi ufanyike haraka

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema hatakubali kucheleweshwa kwa Uchaguzi Mkuu, kutumiwa kwa maslahi ya watu wa kigeni nchini humo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed. AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

Aidha, amesema kuwa suala la Uchaguzi litaamuliwa na wananachi wa Ethiopia na sio watu wa nje, wakati huu akiyashtumu baadhi ya mataifa ya nje kwa kujaribu kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo wakati huu Marekani na Umoja wa Ulaya, wakiishtumu serikali yake kwa ukiukwaji wa haki za binadamu katika jimbo la Tigray.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba, jeshi la shirikisho lilianzisha operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya waasi wa TPLF, utawala wa zamani wa jimbo la Tigray, mkoa wa kaskazini kwenye mpaka na Eritrea.

Mnamo Novemba 28, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alidai ushindi, lakini vurugu zinaendelea. Uhalifu mwingi uliripotiwa. Kila kambi inahusishwa katika uhalifu huo, hali ya kibinadamu ni mbaya na mapigano sasa yanaripotiwa katika maeneo mengi.

Watu milioni 4.5 wanahitaji misaada ya kibinadamu. Katika jimbo la Tigray, mzozo unaoendelea na hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya zaidi.

Kambi za watu waliokimbia makazi yao zimejaa. Mfano wa mji mkuu Mekele, ambapo kuna zaidi ya maeneo 20, wakati mwingine hukaa zaidi ya watu 10,000.

"Tuna shida nyingi za usafi, watu wana njaa," amesema mmoja wa wakimbizi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.