Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Uchaguzi wa wabunge wa Juni 5 waahirishwa Ethiopia

Ethiopia imeahirisha uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika Juni 5, tume ya kitaifa ya uchaguzi imesema Jumamosi hii, ikiongeza kwamba uamuzi huo haupaswi kuzidi wiki tatu.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, Novemba 30, 2021, Adís Ababa.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, Novemba 30, 2021, Adís Ababa. Amanuel Sileshi AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Hapo awali uchaguzi wa wabunge ulipangwa kufanyika mwezi Agosti 2020, lakini uliahirishwa kwa sababu ya janga la COVID-19.

Tangu wakati huo, nchi hii ya pili yenye watu wengi barani Afrika imekuwa ikipambana na vurugu katika mkoa uliojitenga wa Tigray, ambao hautashiriki uchaguzi huo, na pia katika mikoa mingine.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed, aliye madarakani tangu 2018, na Chama chake, wanakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vyama na makundi ya kisiasa ya kikabila yanayodai utawala zaidi kwa mikoa yao.

Birtukan Mideksa, mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya Uchaguzi nchini Ethiopia, "amesema ucheleweshaji katika kufungua vituo vya kupigia kura na kusajili wapiga kura umechelewesha siku yauchaguzi," limeiripoti shirika la habari serikali la FANA.

Birtukan Mideksa amelithibitishia sirika la habari la REUTERS kwamba uchaguzi hautafanyika Juni 5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.