Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Ethiopia: Bunge laidhinisha chama cha TPF na OLA kama makundi ya kigaidi

Chama tawala cha zamani katika jimbo la Tigra, TPF, kiliokuwa kinapambana na vikosi vya serikali y Addis Ababa katika jimbo hilo la kaskazini tangu mwezi Novemba mwaka jana kimewekwa katika makundi ya kigaidi pamoja na kundi lenye silaha la OLA linalodai kulinda watu kutoka jamii ya Oromo, magharibi mwa Ethiopia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Addís Abeba, Februari 3.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Addís Abeba, Februari 3. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unahatarisha kuitumbukiza nchi ya Ethiopia katika vita vikubwa vya wenyewe kwa wenyewe.

Bunge linalodhibitiwa na serikali limepiga kura kwa kauli moja kwa kukiweka chama tawala cha zamani cha TPLF katika jimbo la Tigray na kundi la OLA katika makundi ya kigaidi. Mamlaka inawatuhumu kwa kuchochea ghasia za kikabila, kwa kudhoofisha mamlaka ya serikali ya shirikisho, kwa kuvipa silaha, kufadhili, kutoa mafunzo na kutoa ushauri kwa makundi mengine yenye msimamo mkali.

Kwa upande wa Waziri mkuu Abiy Ahmed, amesema mashambulio ya TPLF na OLA yalipoteza maisha ya maelfu ya watu, na kutaka kuzuia mageuzi ya Abiy Ahmed.

Kulingana na watetezi kadhaa wa haki za binadamu, nakala hii pana inaweza kutumika kama kisingizio cha kushambulia jamii au watu binafsi kiholela. Alhamisi wiki hii Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gedion Timothewos aliahidi kwamba raia wa kawaida hawataathiriwa.

Herman Cohen, naibu waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani alisema nakala hiyo "haikubaliki wakati serikali ingelitazama jinsi ya kubadili mfumo na kutoa msamaha kwa washtumiwa na kuboresha maridhiano."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.