Pata taarifa kuu
LIBYA

Kaimu Waziri mkuu mpya kuapishwa Libya

Waziri Mkuu wa Libya Abdelhamid Dbeibah, ambaye anatarajia kuongoza kipindi cha mpito hadi uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi wa Desemba, anaapishwa leo Jumatatu.

Waziri Mkuu wa Libya Abdul Hamid Dbeibah mbele ya Bunge. Machi 9, 2021 huko Sirte.
Waziri Mkuu wa Libya Abdul Hamid Dbeibah mbele ya Bunge. Machi 9, 2021 huko Sirte. AFP - MAHMUD TURKIA
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja zaidi ya mwezi mmoja baada ya kuteuliwa kwake kama sehemu ya mchakato wa kisiasa uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kuiondoa Libya katika muongo mmoja wa machafuko .

Sherehe hiyo inafanyika kwenye makao makuu ya Bunge  la mpito, yaliyowekwa katika mji wa bandari wa Tobruk mnamo mwaka wa 2014. Mji ho unpatikana  kilomita 1,300 mashariki mwa mji mkuu Tripoli.

Dbeibah kuziunganisha kambi hasimu

Baada ya mgogoro wa kisiasa na machafuko kuikabili nchi hii iliyogawanyika katika kambi mbili - moja mashariki, na nyingine magharibi - Bwana Dbeibah, 61, aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa mpito Februari 5 na maafisa 75 wa Libya kutoka pande zote walikusanyika Geneva chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa, pamoja na Baraza la Rais lenye wanachama watatu.

Serikali yake ya umoja wa kitaifa ilipigiwa kura ya i,ani ya "kihistoria"na wabunge siku ya Jumatano.

Inachukua nafasi ya serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) ya Fayez al-Sarraj, iliyowekwa mnamo mwaka wa 2016 na ambayo ilikuwa na makao yake makuu Magharibimwa nchi na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, na ile ya Abdallah al-Theni - isiyotambuliwa na jamii ya kimataifa -, yenye makao yake makuu huko Cyrenaica , mkoa uliodhibitiwa na majeshi ya Marshal Khalifa Haftar.

Ana kibaruwa kigumu cha kuziunganisha taasisi za nchi hiyo na kuhakikisha kunakuwa uch na kukabidhiana madaraka baada ya uchaguwi wa Desemba 24, wakati kipindi chake cha uongozi kitakuwa kimemalizika.

Serikali ya Dbeibah inaundwa na Mawaziri wakuu wawili, mawaziri 26 na maafisa wakuu sita wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.