Pata taarifa kuu
MISRI

Mfereji wa Suez: Meli Ever Given yarejeshwa majini, shughuli zaanza tena

Mamlaka ya Mfereji wa Suez (SCA) imeangaza  leo Jumatatu "kuanza tena kwa shughuli za usafiri na uchukuzi" katika njia hii kuu ya baharini iliyozuiliwa kwa karibu wiki moja na meli kubwa ya makontena, Ever Given, ambayo ilikuwa bado kando ya mto dakika chache zilizopita.

Picha ya wavuti ya FleetMon iliyopigwa, ambapo unaweza kuona meli ya kubwa ya makontena ya Ever Given, jinsi  imeweza kugeuka, kwenye Mfereji wa Suez, Jumatatu Machi 29, 2021.
Picha ya wavuti ya FleetMon iliyopigwa, ambapo unaweza kuona meli ya kubwa ya makontena ya Ever Given, jinsi imeweza kugeuka, kwenye Mfereji wa Suez, Jumatatu Machi 29, 2021. © FLEETMON VIA REUTERS - FLEETMON
Matangazo ya kibiashara

Osama Rabie, mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez, ametangaza kuanza tena kwa shughuli za uchukuzi na usafiri kwenye mfereji wa Suez," SCA imetangaza katika taarifa leo mchana.

Wakati huo huorais wa Misri Abdel Fattah Al-Sisi amesifu operesheni ya kundolewa kwa meli hiyo.

Kukwama kwa meli hiyo katika Mfereji huo wa kulisababisha msongamano mkubwa wa meli zinazofaa kupita katika mfereji huo

"Kwa kurudisha mambo kuwa katika hali ya kawaida, kwa mikono ya Wamisri, ulimwengu wote unaweza kuhakikishiwa njia ya bidhaa na mahitaji ambazo zinachukuliwa kupitia nji hii ya baharini’ rais wa amenukuliwa akisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.