Pata taarifa kuu
SUDANI

Karthoum yataka upatanishi wa pande nne kuhusu bwawa la Renaissance

Waziri Mkuu wa Sudan ameomba kundi la kimataifa kuchukua nafasi katika mzozo kati ya Misri na Ethiopia juu ya ujazaji wa bwawa la Renaissance. Awamu ya pili ya kujaza bwawa hilo itaanza msimu ujao wa joto.

Bwawa Kubwa la Renaissance kwenye Mto Nile nchini Ethiopia, Septemba 26, 2019.
Bwawa Kubwa la Renaissance kwenye Mto Nile nchini Ethiopia, Septemba 26, 2019. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Wito huu ni ishara tosha ya uhusiano wa karibu  kati ya Khartoum na Cairo dhidi ya mpinzani wake, Ethiopia.

Waziri Mkuu Abdallah Hamdok alitoa ombi lake hilo kwa barua.

Sudan, imesema katika barua yake ya Machi 13, inatoa wito wa kuanzishwa kwa "utaratibu wa upatanishi wa pande nee katika mchakato wa mazungumzo" na Ethiopia. Ili kufanya hivyo, Sudan inautaka Umoja wa Afrika kwanza, kisha Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Marekani.

Kwa kifupi, wazo lake ni kuwafanya waangalizi wa majadiliano hayo kuwa wapatanishi kamili. Lakini ili kufanikisha jambo hilo, kulingana na barua hiyo, kuna ulazima wa "kubadilisha mtazamo" na "kunufaika na uzoefu" uliotokana na mazungumzo ya hapo awali, ambayo yote yalishindwa.

Sudani na Misri waungana dhidi ya Ethiopia

Wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa Sudan alikuwa Cairo, ambapo alikutana na rais wa Misri Abdel Fatah al-Sisi. Wawili hao walionyesha  kuwa wote wanaunga mkono wazo hilo.

Lakini Ethiopia imefutilia mbali hoja hiyo na tayari imesema. Kutokana na uhusiano mbaya na Umoja wa Ulaya na Marekani kwa sababu ya vita huko Tigray, Addis Ababa imebaini kwamba "mifumo iliyopo" inatosha kabisa, hasa mazungumzo ambayo yanaendelea kupitia DRC, ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.Kufikia sasa mazungumzo hayo hayajazaa matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.