Pata taarifa kuu
MSUMBIJI

Mapigano mapya yazuka karibu na mradi wa gesi wa TOTAL nchini Msumbiji

Mapigano yameendelea leo Alhamisi kwa siku ya pili mfululizo nje kidogo ya mji wa Palma, ulio kaskazini mwa Msumbiji karibu na mradi mkubwa wa gesi wa kampuni ya TOTAL, vyanzo viwili vya usalama na mwanadiplomasia mmoja ameliiambia shirika la habari la REUTERS.

Mkoa wa Cabo Delgado unaendelea kukukmbwa na mashambulizi ya wanajihadi.
Mkoa wa Cabo Delgado unaendelea kukukmbwa na mashambulizi ya wanajihadi. ADRIEN BARBIER AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Msumbiji imethibitisha kuwa mji huo ulioko katika mkoa wa Cabo Delgado ulishambuliwa kutoka pande tatu siku ya Jumatano na kwamba vikosi vya usalama vilifanya kazi kubwa ili kurejesha utulivu.

Mji wa Palma uko ndani ya mzunguko wa kilomita 25 ambapo kampuni ya mafuta ya TOTAL imeitaka serikali kutenga "eneo maalum la usalama".

TOTAL kuanzisha tena mradi wa gesi asili

Kabla tu ya shambulio hili jipya, kampuni hii ya mafuta ya Ufaransa ilitangaza Jumatano kuwa itaanzisha tena mradi huu wa gesi asili, ambao uutagharimu dola bilioni 20 (euro bilioni 16.9), kufuatia kuundwa kwa eneo hili la usalama.

Kampuni ya TOTAL haikutoa maelezo zaidi kuhusu shambulio hili jipya.

Jimbo la Cabo Delgado limeendelea kukumbwa na machafuko tangu mwaka 2017 yanayotekelezwa na wapiganaji wa kijihadi wanaohusishwa na kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.