Pata taarifa kuu
DRC-MSUMBUJI-UGAIDI

Makundi ya waasi nchini DRC na Msumbiji yahusishwa na Islamic State

Marekani inasema makundi ya waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchini Msumbiji ni magaidi kutoka nje ya nchi hiyo.

Wanajeshi wa DRC wakiwa katika Operesheni dhidi ya waasi wa ADF Mashariki mwa nchi hiyo.
Wanajeshi wa DRC wakiwa katika Operesheni dhidi ya waasi wa ADF Mashariki mwa nchi hiyo. AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Nchini DRC, kundi la ADF limetajwa kuwa la kigaidi huku Al Ansar al-Sunna, linalofahamika kama Al-Shabaab nchini Msumbiji, yakitajwa kushirikiana na kundi la kijihadi la Islamic State.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imesema viongozi wa makundi hayo, wanashirikiana kwa karibu na wale wa Islamic State na sasa wamekewa vikwazo.

Kundi la ADF limeendelea kusababisha ukosefu wa usalama Mashariki mwa DRC hasa katika Wilaya ya Beni na tangu kuanza kwa mwaka 2021, limesababisha vifo vya mamia ya raia.

Nalo kundi la Ansar al-Sunna, limetekeleza mauaji ya zaidi ya watu 1,300 nchini Msumbiji tangu Oktoba mwaka 2017.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.